Mchezaji wa Yanga ametumia ukurasa wake wa Instagram kutoa taarifa kwa mashabiki zake na wa club ya Yanga kuhusu tetesi ambazo zinasambaa kwamba yeye anataka kuhamia club ya Simba.
Kwenye hiyo taarifa aliandika hivi, “Kuweka wazi kwa mashabiki wangu na mashabiki wa Yanga, habari zinazotoka kwenye radio na magazeti kwamba nataka kujiunga na club ya Simba. Kuna mtu anaandika hizi habari na sio kweli wala sijasema kwenye mdomo wangu. Nipo vizuri hapa Yanga na nina furaha. Nina mpango wa kumaliza mkataba wangu wote hapa na maisha yangu ya baada mungu ndie anajua.”
No comments:
Post a Comment